Shughuli ya kitaifaya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli inaendelea katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Shughuli hiyo inahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi, wageni kutoka nchi mbalimbali pamoja na wenyeji wa Mkoa wa Dodoma na mikoa jirani wakiongozwa na Rais, Samia Suluhu Hassan.
Mwili wa Dkt. Magufuli unaagwa kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri, ambapo majira ya asubuhi uliagwa katika viwanja vya Bunge na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tayari gwaride maalum lililoandaliwa na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya kuaga mwili wa Dkt. Magufuli limemaliza kutoa heshima za mwisho.