Dkt. Magufuli atajwa kiongozi aliyejiweka tayari

0
320

Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro lililopo mkoani Dar es salaam Dkt Alister Makubi, amemwelezea Dkt John Magufuli aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa alikuwa kiongozi ambaye alijiweka tayari kwa maisha ya kiroho.

Akitoa mahubiri wakati wa Misa Takatifu ya kumuombea Dkt Magufuli, Dkt Makubi amesema wakati wa uhai wake kiongozi huyo aliwasihi Watanzania kuwa tayari kufanya mambo kwa haraka na kujiweka tayari kwa maisha ya baadaye baada ya kuondoka hapa duniani.

Amesema huu ni wakati kwa Watanzania kusherehekea maisha ya Dkt Mafufuli kwa kufuata yale yote mema aliyoyatenda kiongozi huyo aliyewapenda sana Watanzania.

Baada ya Misa hiyo ya kumuombea Dkt Magufuli, mwili wake umepelekwa katika uwanja wa Uhuru mkoani Dar es salaam  ambapo shughuli ya kuuaga itafanyika leo na kesho kwa mkoa huo.

Mwili wa Dkt Magufuli utazikwa Chato mkoani Geita tarehe 26 mwezi huu