Misa takatifu ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli inaendelea hivi sasa katika kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay mkoani Dar es salaam.
Misa hiyo inahudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Mjane wa Dkt Magufuli, Mama Janeth Magufuli.
Kabla ya kuanza kwa Misa hiyo, mwili huo ulitolewa Ikulu jijini Dar es Salaam kuelekea kanisa hapo ambapo njiani wananchi mbalimbali walijitokeza kumuaga.
Mara baada ya misa hiyo, mwili huo utapelekwa katika Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya ya kuagwa.