Wajasiriamali wamlilia Dkt Magufuli

0
223

Wajasiriamali wanaojihusisha na biashara ya maua katika eneo la Namanga mkoani Dar es salaam, wameungana kutengeneza bango maalum la kumkumbuka Dkt John Magufuli aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wajasiriamali hao wamesema kifo cha Dkt Magufuli ni pigo kwa Wajasiriamali wa aina zote, kutokana na mchango wake mkubwa kwa Wajasiriamali hao.

“Kifo cha Magufuli kimetuumiza wengi, kwani alikuwa mstari wa mbele kuwatetea Wajasiriamali pale walipofukuzwa katika maeneo mbalimbili ya kujitafutia mkate wao wa kila siku.” wameeleza Wajasiriamali hao.

Aidha wamebainisha kuwa, eneo hilo ni moja ya maeneo ambayo mke wa Dkt Magufuli, Mama Janeth Magufuli alikuwa akitembelea mara kwa mara na kuwaunga mkono kwa kununua maua.

Pia wameeleza kuwa wana imani na Rais mpya Samia Suluhu Hassan kuwa atapigania haki za Wajasiriamali, kama alivyofanya Rais Magufuli.

“Tunaamini Mama Samia Suluhu Hassan atayaendeleza mazuri ya Dkt Magufuli kwa sababu alifanya naye kazi kwa karibu kwa muda wa miaka mitano.”wameongeza Wajasiriamali hao.