Rais Magufuli kuzikwa Machi 25

0
193

Rais Samia.Suluhu Hassan amesema mazishi ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli yatafanyika Machi 25, 2021 huko Chato mkoani Geita.

Akizungumza Ikulu mkoani Dar es salaam baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia amesema kesho mwili wa Dkt Magufuli utafanyiwa misa katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay na baadaye utapelekwa kwenye uwanja wa Uhuru.

Siku ya Jumapili Wakazi wa mkoa wa Dar es salaam watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho na siku ya Jumatatu wakazi wa Dodoma nao watapata nafasi hiyo.

Wakazi wa mkoa wa Mwanza nao watapata nafasi ya kuaga Machi 23, na Machi 24 itakuwa ni familia na wakazi wa mkoa wa Geita.