Mbatia atoa neno msiba wa Magufuli

0
335

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, – James Mbatia, ametoa rai kwa Watanzania kuwa wamoja na kushikamana katika kipindi hiki cha msiba wa Rais Dkt John Magufuli.

Mbatia ametoa rai hiyo mkoani Dar es salaam wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari na kuongeza kuwa hiyo ndio njia pekee ya kumuenzi Rais Magufuli.

Amesema katika kipindi hiki cha maombolezo, bendera ya Chama cha NCCR Mageuzi itapepea nusu mlingoti na kwamba chama hicho kipo na Watanzania wote katika kuomboleza kifo cha Rais Magufuli.