Salamu za pole kufuatia kifo cha Rais Dkt. Magufuli

0
207

Viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika wametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021.

Rais Dkt. Magufuli alifariki kutokana na maradhi ya moyo ambapo alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam kuanzia Machi 14.

Kufuatia kifo hicho, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ametangaza siku 14 za maombolezo ambapo bendera zote zitapepea nusu mlingoti.

Hapa chini ni baadhi ya salamu za viongozi hao;