Wanafunzi wachunguzwa kwa vitendo vya ngono shuleni

0
223

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke mkoani Dar es salaam, – Lusubilo Mwakabibi amesema Wanafunzi wanne wa shule ya msingi Toangoma wanachunguzwa kufuatia  tuhuma za utovu wa nidhamu na ukiukaji wa maadili ya shule.

Akitoa taarifa hiyo kwa Waandishi wa habari mkoani Dar es salaam, -Mwakabibi amesema Wanafunzi hao wamebainika kuwa na rekodi mbaya wakiwa  shuleni, jambo ambalo limeifanya halmashauri ya Temeke kuwachunguza.

Amesema lengo la kuwachunguza Wanafunzi hao ni kutunza heshima ya  shule ya msingi ya Toangoma, ambayo kumekuwa na taarifa za Wanafunzi kujihusisha  na mambo ambayo hayafai kwa jamii kulingana na umri wao ikiwa ni pamona na kujihusisha na vitendo vya ngono.

Mwakabibi amewaomba Wazazi na Walezi wa Wanafunzi wanaosoma shuleni hapo kupitia kamati za Wazazi, kufuatilia  malezi na makuzi ya watoto wao.

Amesema sababu inayochangia kushindwa kudhibitiwa kwa Wanafunzi katika shule hiyo ya msingi ya Toangoma ni ongezeko kubwa la Wanafunzi.