Watafiti wakuna vichwa tiba magonjwa yasiyoambukiza

0
225

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Dorothy Gwajima amesema Serikali inaendelea na tafiti ambazo zikifanikiwa zitawawezesha wananchi kutumia tiba asili katika kutibu magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza ikiwemo saratani.

Dkt Gwajima amesema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road mkoani Dar es salaam.

Kutokana na kuwepo kwa gharama kubwa za matibabu Dkt Gwajima ameeleza kuwa, Serikali inaandaa mkakati wa kuwezesha upatikanaji wa bima ya afya kwa watu wote, ili kila mmoja apate matibabu bila usumbufu.

Hata hivyo amesema Serikali imekuwa ikitoa msamaha wa gharama za matibabu kwa watu wanaoonekana kuwa hawana uwezo wa kugharamia matibabu hasa ya saratani.