Simba VS Al Merreikh kuchezwa bila Mashabiki kwa Mkapa

0
278

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limeiandikia barua TFF ya kuzuia Mashabiki kuingia uwanjani wakati wa mchezo wa Raundi ya nne ya hatua ya Makundi ya ligi ya Mabingwa barani Afrika baina ya wenyeji Simba dhidi ya Al Merreikh ya Sudani.

Wakati michuano hiyo inaanza CAF iliiruhusu Simba Kucheza ikiwa na mashabiki elfu 30 tu ikiwa ni hatua ya shirikisho hilo kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya Ugonjwa wa Corona.