Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kutoamini mitandao ya kijamii ambayo baadhi ya watumiaji wake huchapisha taarifa za uongo.
Waziri Mkuu ametoa rai hiyo mkoani Njombe mara baada ya kushiriki swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Wilaya ya Njombe ambapo amewataka Watanzania kuwa watulivu kwa kuwa Rais Dkt. John Magufuli yupo salama na anaendelea na majukumu yake.
Amewataka Watanzania kuendelea kuliombea Taifa, huku viongozi wakitakiwa kukemea roho za chuki na kuhimiza kupendana.