Mrema wa CHADEMA akanusha uzushi wa kifo dhidi yake

0
129

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema kuwa yeye ni mzima wa afya.

Mrema amesema hayo baada ya kusambaa taarifa mitandaoni zikidai kuwa amefariki dunia akiwa nchini Afrika Kusini.

“… nimeanza kupokea salamu za pole, wengine Watanzania wakienda nyumbani kwangu, wakienda kijijini kwetu Moshi. Nachopenda kuwathibitishia mimi siumwi,” ameeleza Mrema kwenye taarifa yake kwa umma.

Ameongeza kuwa hajasafiri kwenda Afrika Kusini na kwamba mara ya mwisho kutoka nje ya nchi ilikuwa mwaka 2020.