Wanawake wang’ara zaidi sekta ya habari

0
236

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajibi Mukajanga amesema tangu waanze kutoa tuzo za umahiri, kwa miaka mitatu mfululizo waandishi wa habari wanawake wamekuwa wakifanya vizuri zaidi kila mwaka.

Mukajanga amesema kujituma katika kazi zao ndiyo sababu kuu ya matokeo hayo na kwamba licha ya kuwa nyingi ni tuzo za kipengele kimoja kimoja, lakini pia mshindi tuzo za jumla kwa kipindi cha miaka mitatu ni mwanamke.

Amebainika hayo katika mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari ya kuwajengea uwezo wa kuibua habari za ubunifu pamoja na vigezo vikuu vinavyotumika kushindanisha taarifa za habari katika mashindano ya tuzo za umahiri wa habari nchini ambapo waandishi wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na taaluma zao ili kuweza kusaidia jamii yao.