Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Othman Masoud Sharif amesema kuwa Hayati Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa muumini wa umoja na kwamba serikali italisimamia hilo ili kumtendea haki.
Sharif amesema hayo mapema leo asubuhi wakati akizugumza na wananchi waliofika katika dua ya kumuombea Maalim Seif ambaye alifariki dunia Februari 17, 2021 akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Katika hatua nyingine amesema kuwa atashirikiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi kuhakikisha wanaikwamua Zanzibar kutoka hapo ilipo sasa, na kwamba huu ni wakati wa kutazama mbele na kuacha makando kando ya nyuma.
Sharif aliteuliwa kushika wadhifa huo Machi Mosi 2021.