Kamati za Bunge kuanza vikao Machi 8

0
161

Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge la 12, vinatarajia kuanza Machi 8 hadi 26 mwaka huu kabla ya kuanza kwa mkutano wa Bunge Machi 30 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Bunge jijini Dodoma imeeleza kuwa, katika kipindi hicho Kamati hizo.zitakuwa na kazi ya kupokea mapendekezo ya Serikali kuhusu mpango, kiwango na ukomo wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022.

Shughuli nyingine ni Wajumbe wa kamati za kisekta kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi iliyotengewa fedha kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, shughuli nyingine ni uchambuzi wa taarifa za uwekezaji uliofanywa na Serikali kupitia mashirika, taasisi na kampuni ambazo Serikali ina hisa pamoja na kukagua shughuli za uwekezaji zilizofanywa na Serikali.