DC Arusha Mjini akagua mradi wa maji wa bilioni 520

0
179

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini, Kenani Kihongosi amewataka madiwani na watendaji kata kuwaeleza wananchi hatua nzuri iliyofikiwa katika utekeleza wa mradi wa maji pamoja na mambo mengine makubwa yanayofanywa na serikali kuwanaufaisha wananchi.

Kihongosi amesema hayo leo wakati wa ziara ya kikazi kukagua miradi wa maji wa bilioni 520 akiambatana Mstahiki Meya, Maximillian Iraghe, Madiwani wa Jiji la Arusha na watendaji wa kata za jiji hilo.

Aidha, amewipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA) na kuwaagiza wakamilishe mradi kwa wakati ili wananchi wafurahie matunda ya Serikali yao.