Naibu Waziri Ulega: Tuongeze ubunifu

0
130

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega amewataka waandaaji wa mashindano ya kimataifa ya Kilimanjaro Marathon wawe wabunifu na kuongeza vionjo vipya kwenye mashindano hayo ili kuwavutia watu wengi zaidi kuja kushiriki mashindano na kuja kujionea vivutio vizuri vilivyopo katika mkoa wa Kilimanjaro na taifa kwa kwa ujumla.

Naibu Waziri Ulega amesema hayo alipokuwa akifunga mashindano ya mbio za Kili Marathon yaliyofanyika Uwanja wa Ushirika Manispaa ya Moshi.

“Ninyi kama wataalamu wenye uzoefu, angalieni na muongeze ubunifu ili kuboresha mashindano haya, wanapokuja watu hapa uchumi uendelee kukua zaidi ambapo wajasiriamali waendelee kupata pesa zaidi na wenye kuuza baishara ndogondogo waendelee kupata pesa zaidi tujenge uchumi wetu,” amesema Ulega.

Pia amewataka waandaaji wa mashindano hayo kuhakikisha kuongeza ubunifu na yaweze kutangazika zaidi duniani kote ili kuwavuta wakimbiaji wengi wenye majina makubwa duniani waje kushiriki mashindano hayo.

Aidha, Naibu Waziri Ulega amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaonesha Watanzania namna nzuri ya uwekezji na fursa za kibiashara katika Taifa letu bado zipo wazi kwa wawekezaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Moshi Rajabu Kundya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Anna Mughwira ameishukuru Serikali kupitia wizara yenye dhamana ya michezo kwa kusema mashindano hayo yamekuwa chachu ya kuwakutanisha wananchi kutoka mikoa mingine na mataifa mbalimbali kwa kuwa zimeshiriki zaidi ya nchi 55.

Wataalamu wa afya wanehakikisha akili safi daima hukaa kwenye mwili safi, na mwili safi ni ule ambao haujachokonolewa na maradhi na namna pekee ya kuulinda mwili ni kufanya mazoezi na kulinda afya ya mwili na akili, hii ilikuwa ni fursa muhimu ambapo amewasihi Watanzania tuendelee kufanya mazoezi kujiandaa na mashindano yajayo.

Naye Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Irene Mtiganzi ambao ni moja ya wa dhamini wa mashindano amesema kampuni yao inajivunia kuwa na mchango katika kukuza utalii wa michezo nchini hatua inayosaidia kuongeza watalii wa ndani nan je ya nchi katika viutio mbalimbali vilivyopo katika mkuo huo.

Mshindi wa kwanza katika mbio za km 42 kwa wanaume na wanawake amepata zawadi ya Shilingi milioni 4,100,000 kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo na kuongezewa kiasi cha Shilingi 1,500,00 ikiwa motisha kwa Watanzania waliofanya vizuri kwenye mashindano hayo na kufanya jumla ya fedha walizopokea jkufikia kiasi cha Shilingi 5,600,000.

Mashindano ya Kilimanjaro marathon ya mwaka huu ni ya 19 kufanyika tangu kuanzishwa kwake 2003 ambayo yameshirikisha wachezaji zaidi ya elfu 12 kutoka nchi zaidi ya 55 ambapo Watanzania wamefanya vizuri katika mbio za km 42 kuanzia mshindi wa kwanza ambaye ni Augustino Sule aliyekimbia kwa 2:18:04 kwa upande wa wanaume huku kwa upande wa wanawake Watanzania wameongoza kuanzia mshindi wa kwanza ambaye ni Jackline Sakilu aliyekimbia kwa 02:45:44 hadi nafasi ya tisa wakati nafasi ya 10 imechukuliwa na Dominic Kremer raia wa Netherland.