Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Paul Kagame amemtangaza Dkt. Peter Mathuki kuwa Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo.
Dkt. Mathuki ambaye ni Mkenya ni mtaalamu wa Uchangamano wa Kikanda, pia aliwahi kuwa Mbunge wa Afrika Mashariki (EALA) ambapo alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Utawala Bora
Amefanyakazi na Shirika la Kimataifa la Wafanyakazi (ILO) pia ni mtu ambaye alishiriki katika hatua za kuleta Soko la Pamoja la Africa Mashariki (AfCFTA)