Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu -Sera na Uratibu – Profesa Faustin Kamuzora amesema suala la kuweka mazingira bora ya kufanya biashara na uwekezaji ni la lazima kwa sababu serikali ina hisa katika kila biashara inayoanzishwa nchini.
Akizungumza baada ya kikao cha kwanza cha kamati ya mazingira ya biashara jijini Dar Es Salaam, Profesa Kamuzora ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati hiyo amesema mazingira bora ya biashara yataiwezesha sekta binafsi kuanzisha biashara nyingi na serikali kuongeza mapato.
Naye kaimu katibu mtendaji wa baraza la taifa la Biashara- TNB- Oliva Vegula amesema ni muhimu kwa sekta ya umma na sekta binafsi kushikamana na kushirikiana katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.