Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ametangaza siku tatu za maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.
Taarifa ya Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kuwa Maombolezo hayo yaanza leo Tarehe 17 Februari, 2021 na kwamba bendere zote zitapepea nusu mlingoti.
Taarifa hiyo ya Ikulu pia imeambatana na salamu za pole kwa Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, Familia ya Marehemu na watanzania wote.
“ Nimepokea kwa Masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mhe. Malim Seif Sharif Hmad aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar. Natoa pole kwa Rais wa Zanzibar Mhe.Dkt. Mwinyi, Fmilia, wazanzibarwanachama wa ACT-Wazalendo na Watanzania wote. Mungu amuweke mahala pema peponi, Amina”.Amesema Mhe. Rais Magufuli