Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi ametangaza kifo cha aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.
Rais Mwinyi amesema kuwa Maalim Seif amefariki leo Jumatano Saa 5 Asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kufuatia kifo hicho Rais Dkt. Mwinyi ametangaza siku saba za maombolezo na kuagiza Bendera zote zipepee nusu mlingoti.