Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Korogwe Kwame Daftari amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Februari 16, 2021, Hospitalini jijini Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa tangu Januari 24, 2021.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Kasongwa amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.
“Habari za usiku, Wilaya ya Korogwe tumepata msiba mkubwa muda huu wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Kwame Daftari” ulisomeka ujumbe wa Mkuu wa wilaya kwa wana Korogwe.
Hata hivyo ujumbe huo haukutaja sababu za kifo cha Mkurugenzi huyo.