Kilangi ahamasisha umuhimu wa kurasimisha ardhi

0
193

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), John Kilangi amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuhamasisha wananchi kurasimisha ardhi ili kuondoa migogoro na kuwawezesha kutumia hatimiliki kujikwamua kiuchumi ikiwemo kuvutia uwekezaji.

Kilangi ameyasema hayo leo, Februari 9, 2021 wakati wa ziara ya Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kujionea maendeleo yaliyofikiwa katika urasimishaji ardhi Zanzibar kufuatia MKURABITA kujenga uwezo wa kuwezesha utekelezaji wa mpango huo wa urasimishaji.

MKURABITA inawia kushirikiana na wizara hiyo ili kuleta ukombozi wa kiuchumi kwa wananchi.