Afrika Kusini yasitisha chanjo ya Corona

0
174

Serikali ya Afrika Kusini kupitia Waziri wa Afya, Zweli Mkhize imeagiza kusitishwa kwa utoaji wa chanjo ya Oxford-AstraZeneca inayotolewa kwa ajili ya virusi vya COVID-19 aina ya B. 1.351.

Agizo hilo limefikiwa baada ya chanjo hiyo iliyofanyiwa majaribio kwa watu 2,000 kutoa majibu yasiyoridhisha (minimal protection).

Waziri Mkhize ameongeza kuwa wameamua kusitisha utoaji wa chanjo hiyo ambayo Afrika Kusini ilipata dozi milioni moja ambazo zilipangwa kutolewa kwa watoa huduma za Afya kwanza ili kuruhusu wanasayansi kufanya uchunguzi zaidi juu ya uwezo wa chanjo hiyo katika kupambana na aina hii mpya ya virusi vya Corona.

Kwa kipindi hiki serikali ya nchi hiyo itaendelea kutoa chanjo zilizotengenezwa na kampuni nyingine kama Johnson & Johnson na Pfizer

Hadi sasa Afrika Kusini imerekodi maambukizi milioni 1.5 ya COVID-19 na vifo zaidi ya 45,000.