Aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu katika Chama cha Wafanyakazi na Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Sospeter Omollo amefikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu akikabiliwa na Mashitaka 48 ikiwemo shitaka la kutakatisha fedha zaidi ya Shilingi milioni mia nne.
Omollo amefikishwa katika mahakama hiyo nakusomewa mashitaka yanayomkabili na waendesha mashtaka wa TAKUKURU Hassan Dunia na Kibwana Njau mbele ya Hakimu Mwandamizi ya makahama hiyo Yusto Ruboroga.
Awali akimsomea mshitakiwa huyo Mashitaka yanayomkabili, Mwendesha Mashitaka Dunia amedai katika shitaka la 1 hadi la 46 mshitakiwa huyo anakabiliwa na makosa ya kughushi hundi 46 zenye thamani ya zaidi shilingi milioni mianne makosa ambayo anadaiwa kuayatenda kwa nyakati tofauti kati ya Septemba 22, 2015 na Juni 5, 2017 katika benki ya BOA tawi la Ilala iliyopo Jijini Dar es Salama.
Katika shtaka la 47 na la mwisho Wakili huyo amedai kuwa mshtakiwa huyo akiwa mtumishi aliyeaminiwa kama mhasibu wa TALGWU anadaiwa kutenda kosa la ubadhirifu nakutakatisha fedha makosa ambayo anadaiwa kuyatenda kati ya September 22, 2015 na Juni 5, 2017.
Baada ya maelezo hayo Wakili wa Kibwana Njau amedai kuwa upepelezi wa shauri hilo umekamilika na kiuomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili Mshitakiwa kusomewa maelezo ya awali.
Hata hivyo mshitakiwa huyo amekana Mashtaka yake na amepelekwa gerezani baada ya Hakimu Ruboroga kudai kesi ya utakatishaji fedha haidhaminiwi kwa mujibu wa sheria.
Kesi hiyo imeahirishwa Hadi Februari 16 mwaka huu kwa ajili ya Mshitakiwa huyo kusomewa maelezo ya awali.