Rais Dkt. John Magufuli amesema shamba la miti Chato alilolizindua hii leo litaitwa shamba la miti Silayo, ikiwa ni kutambua mchango mkubwa wa kamishna wa uhifadhi wa TFS Profesa Dos Santos Silayo.
Akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa shamba hilo, Rais Magufuli amesema kazi iliyofanywa kwenye shamba hilo ni kubwa na kwamba anatambua mchango wa kamishna Silayo katika mafanikio hayo.
Rais Magufuli amesema hakuwahi kufikiria kama eneo hilo linaweza kuota miti lakini jitihada zinazofanywa TFS katika kurejesha uoto huo.
“Natambua kazi kubwa iliyofanywa na TFS katika eneo hili na kwa mamlaka niliyonayo natamka kuwa shmba hili litaitwa Silayo Forest ili kutambua mchango wa kamishna Silayo katika uhifadhi”, amesema Rais Magufuli
Rais Dkt John Magufuli amezindua shamba hilo la pili kwa ukubwa hapa nchini ambalo limerejesha uoto wa asili wa maeneo ambayo yaliharibiwa na wananchi.