Rais wa Ethiopia Sahle- Work Zewde amewasili Tanzania

0
191

Rais wa Ethiopia Sahle- Work Zewde amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Geita wilayani Chato Mkoani Geita na kupokelewa na mwenyeji wake Rais DKT John Magufuli

Rais Zewde amewasili na Ndege aina ya BOEING 737-800 ya shirika la Ndege la ETHIOPIA majira ya saa nne kasorobo asubuhi.

Baada ya kuwasili katika uwanja huo wa ndege Rais wa Tanzania DKT Magufuli ameongozana na mgeni wake kuelekea ikulu ndogo kwa mazungumzo ya faragha (tete-a-tete)

Katika hatua nyingine Marais hao wamepeana zawadi kabla ya kuanza mazungumzo hayo.