Rais wa Ethiopia kufanya ziara nchini

0
178

Rais Sahle-Work Zewde wa Ethiopia, kesho atakuwa na ziara ya kikazi ya siku moja nchini yenye lengo ya kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Ethiopia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba kabudi amesema Rais Sahle atawasili katika uwanja wa ndege wa Geita kesho majira ya saa nne asubuhi, na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Magufuli.

Akiwa hapa nchini pamoja na mambo mengine, Rais huyo wa Ethiopia atakuwa ma mazungumzo na Rais Dkt Magufuli.

“Nitumie fursa hii kutoa muhtasari wa uhusiano na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ethiopia, Tanzania na Ethiopia zimekuwa na mahusiano ya muda mrefu na ushirikiano mzuri kwa muda wote huo, na uhusiano huu unatokana na msingi mzuri uliojengwa na muasisi wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,” amesema Profesa Kabudi.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amewaomba Wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kumpokea mgeni huyo kama ilivyo desturi yao.

“Niwaombe wana Geita tujitokeze kwa wingi kuanzia majira ya saa 12, tuweze kumpokea mgeni ambaye atakuja katika mkoa wetu wa Geita, mgeni huyo ni Rais wa Ethiopia ambaye majira ya saa nne asubuhi atakuwa ameshawasili,” amesema Mhandisi Gabriel.