Wakazi wa Liganga watumia mifuko ya taka kutengeneza Daraja

0
193

Wakazi wa mtaa wa Liganga uliopo jijini Dodoma wamelazimika kutumia mifuko yenye taka ngumu kama kifusi cha kutengeneza daraja linalojulikana kama daraja la dhambi, kwa lengo la kuwawezesha kupata mawasiliano baada barabara hiyo kukatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ameshuhudia wananchi wakipata kadhia hiyo wakati alipofika kufanya zoezi la upandaji miti katika eneo hilo hali inayomlazimu kutoa maagizo kwa wakala wa barabara (TARURA) Mkoa wa Dodoma kuanza zoezi la ujenzi wa daraja hilo ndani ya siku tano.

Wakazi wa eneo hilo wamesema wamefanya hivyo kutokana na watoto wao kushindwa kwenda shule upande wa pili kutokana na kuaribika kwa daraja hilo.

Aidha Dkt. Mahenge akiwa na viongozi wa jiji ameongoza zoezi la upandaji miti katika barabara mbalimbali za jiji la Dodoma.