Brigedia Jenerali Mstaafu Maganga aagwa Tabora

0
181

Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga, umeagwa katika eneo la Ipuli mkoani Tabora.

Akiongoza misa ya kuaga mwili huo, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Magharibi Tabora Dkt Isack Kisiri Laizer amehimiza kuenziwa kwa mambo yote mazuri yaliyofanywa na Brigedia Jenerali Mstaafu Maganga wakati wa uhai wake.

Akitoa salamu za rambirambi, Mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt Philemon Sengati amemuelezea Brigedia Jenerali Mstaafu Maganga kuwa alikuwa mlezi wa watu aliyewatumikia na alilitumikia Taifa kwa uaminifu na uadilifu.

Mwili wa Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga aliyefariki dunia usiku wa kuamkia hii leo katika hospitali ya Jeshi ya Milambo mkoani Tabora,  umesafirishwa kwenda jijini Dar es salaam kwa taratibu za mazishi.