Bumbuli walilia kiwanda cha chai Mponde

0
185

Mbunge wa jimbo la Bumbuli lililopo mkoani Tanga, -January Makamba amemuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwasaidia wakulima wa zao la chai wa jimbo hilo kumaliza tatizo la kusimama kwa uzalishaji kwenye kiwanda cha Mponde.

Makamba ametoa ombi hilo wakati wa kikao kilichoshirikisha Wadau wa zao la Mkonge kilichofanyika jijini Tanga.

Amesema Wakulima wa zao la chai katika jimbo hilo la Bumbuli walifarijika wakati Waziri Mkuu Majaliwa alipofanya ziara mahususi kwa ajili ya kutatua mgogoro kwenye kiwanda hicho cha chai cha Mponde.

Amesema ni vema Serikali ikasaidia kufikia tamati ya suala hilo kama ilivyoahidi hapo awali.

Makamba ameshauri kama kuna changamoto zinazozuia kufunguliwa kwa kiwanda hicho cha chai cha Mponde, Serikali ichukue hatua ya kuzitatua ikiwa ni pamoja na kuwakaribisha Wawekezaji ambao wataweza kukiendesha.