Rais Donald Trump wa Marekani na mkewe Melania, tayari wameondoka katika Ikulu ya Marekani, zikiwa zimesalia saa chache kabla Joe Biden kuapishwa kuwa Rais wa 46 wa nchi hiyo.
Trump ameelekea katika eneo la Kambi ya kijeshi ya Andrews, ambapo ndipo atakapotoa hotuba yake ya mwisho.
Maafisa mbalimbali wa Ikulu ya Marekani pamoja na watu kadhaa wameshuhudia helikopta ya Wanamaji iliyombeba Trump na Mkewe ikiondoka katika eneo hilo.
Makamu wa Rais Mteule wa Marekani, – Kamala Harris naye ataapishwa pamoja na Joe Biden, akiwa ni Mwanamke wa Kwanza kushika wadhifa huo.