Serikali mkoani Iringa imewakabidhi rasmi watoto pacha walioungana moyo Dorcas na Dorin Lemshungu kundai kwa Masista wa Theresina katika kituo cha kulea watoto yatima Tosamaganga kilichopo wilayani Iringa.
Pacha Dorcas na Dorin walizaliwa mwezi Julai mwaka 2020 na kupelekwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na ikagundulika kuwa wanatumia moyo mmoja kwa hiyo ni vigumu kutenganishwa.