Saa za Trump White House zayoyoma

0
406

Sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Marekani, -Joe Biden zinatarajiwa kufanyika kesho majira ya mchana kwa saa za Marekani.
 
Mwanamuziki Lady Gaga anatarajiwa kuimba wimbo wa Taifa hilo katika hafla hiyo ambayo inatarajiwa kuhudhuriwa na watu wachache.
 
Makamu wa Rais Kamala Harris ataapishwa kabla ya Biden kuapishwa na kuhutubia.
 
Ulinzi umeimarishwa maradufu katika jiji la Washington DC ambapo maelfu ya askari wameongezwa katika jiji hilo.
 
Rais Mteule Biden na Makamu wa Rais mteule Kamala wanatarajiwa kuwasili jijini Washington hii leo kwa ndege.
 
Aidha baadae leo ibada maalum inatarajiwa kufanyika kuwakumbuka maelfu ya watu waliofariki duniani baada ya kuugua Corona nchini Marekani.