Diamond agoma kuzungumzia mambo binafsi

0
362

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Wasafi Media Naseeb Abdul, maarufu kwa jina la Diamond Platinumz amekataa kuzungumzia habari ambazo zimekuwa zikizungumzwa kwenye mitandao mbalimbali jamii zinazoihusu familia yake.

Akijibu swali la mmoja wa Waandishi wa habari jijini Dar es salaam aliyetaka kujua majina yake halisi atakayokuwa anayatumia kwa sasa, Diamond amesema suala hilo atalizungumzia siku nyingine.

“Masuala ya chumbani hayapaswi kuwekwa hadharani, hivyo suala hili nitalizumgumzia siku nyingine ila kwa sasa tuzungumze juu ya tamasha lililoko mbele yetu kwa ajili ya Watanzania,” amesema Diamond.

Aidha, Diamond amewataka Watanzania kuyapa kipaumbele mambo yenye maslahi kwa Taifa badala ya kukaaa mitandaoni kufuatilia vitu ambavyo havina tija kwa Taifa.

Kauli ya Msanii huyo imekuja zikiwa zimepita siku chache baada ha kuibuka kwa sintofahamu juu ya baba halisi wa Msanii huyo.