Mkuu wa mkoa wa Tanga, – Martine Shigella ametoa wito kwa Wakulima, Wafanyabiashara na wenye Kampuni binafsi kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano maalum wa Wadau wa Mkonge, unaotarajia kufanyika jijini Tanga hapo kesho na kuongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mkutano huo pamoja na mambo mengine una lengo la kujadili hatua za kufufua zao la Mkonge hapa nchini.
Zao la Mkonge ni miongoni mwa mazao Saba ya kimkakati nchini na Serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni mia saba kwa ajili ya ufufuaji wa zao hilo.