Uchumi wa China umekuwa kwa kiwango ambacho hakikutarajiwa, licha ya virusi vya Corona kuzuka katika mji wa Wuhan, hali iliyoathiri uchumi wa nchi hiyo.
Uchumi wa China umekuwa kwa asilimia 2.3 katika kipindi cha mwezi septemba hadi Desemba mwaka 2020, na hivyo kuifanya nchi hiyo kuongoza duniani kwa ukuaji wa uchumi.
Shughuli za biashara na uzalishaji mali zililazimika kusimama nchini China, baada ya nchi hiyo kukumbwa na Corona na baadaye Taifa hilo likafanikiwa kudhibiti virusi hivyo na kuendelea na uzalishaji mali.