Solskjaer asema kikosi chake bado imara

0
362



Meneja wa Manchester United, – Ole Gunnar Solskjaer amesema kikosi chake kimepoteza nafasi ya kuifunga Liverpool baada ya timu hizo kutoka suluhu katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa kwenye dimba la Anfield.


Liverpool ambayo ilicheza bila uimara katika safu ya ulinzi huku pia ikiwakosa baadhi ya viungo wake akiwemo Jordan Henderson na Fabinho,  ilimiliki mpira kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha kwanza lakini United wao wakapoteza nafasi nyingi za wazi za kupata ushindi katika mchezo huo.


Solskjaer anasema wangeweza kuondoka na ushindi kwenye dimba la Anfield lakini walikuwa wakicheza na timu bora huku pia akikimwagia sifa kikosi chake kwamba kimebadilika na kina muelekeo mzuri katika msimu huu na ana imani watafanya vizuri katika michezo inayofuata.


Suluhu ya jana inawafanya United kuwa timu ya kwanza kuizuia Liverpool kupata bao kwenye dimba la Anfield tangu walipofanya hivyo Man City mwezi Oktoba mwaka 2018, lakini Liverpool wakiendeleza rekodi ya kutopoteza katika michezo 68 ya Ligi Kuu wakiwa nyumbani wakivuna alama 178 kati ya 204 ambazo wangevuna katika michezo hiyo.


United wanaendelea kusalia kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England wakiwa na alama 37 huku nafasi ya pili ikikaliwa na Man City wenye alama 35, Leicester City wakiwa katika nafasi ya tatu na alama 35 pia, wakati Liverpool wakiporomoka hadi katika nafasi ya nne wakiwa na alama 34.