Makamu wa Rais aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Chamwino

0
211

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, leo ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichoketi Ikulu Chamwino mkoani Dodoma ambacho kimejadili masuala matatu muhimu.

Pamòja na mambo mengine, kikao hicho kimepitia mapendekezo ya mpango wa Tatu  wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano.

Kikao hicho pia kimepitia mapendekezo ya mwongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti  ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 na mapendekezo ya mpango wa maendeleo ya Taifa wa mwaka 2021/2022.