Shule 10 zilizofanya vizuri mtihani wa kidato cha nne

0
253

Shule ya sekondari ya St Francis imeongoza katika orodha ya shule 10 źilizofanya vizuri mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka 2020.

Taarifa ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) imeitaja shule ya sekondari ya Ilboru kuwa ndio iliyoshika nafasi ya pili ikifuatiwa na shule ya sekondari ya Canossa.

Taarifa hiyo.iliyotolewa jijini Dar es salaam mbele ya Waandishi wa habari na Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt Charles Msombe imeitaja shule ya sekondari ya Kemebos kushika nafasi ya nne ikifuatiwa na shule ya sekondari ya Wasichana ya  Bethel Sabs na shule ya sekondari ya wavulana ya Feza yenyewe imeshika nafasi ya sita.

Nafasi ya saba imeshikiliwa na shule ya sekondài ya Ahmes, St Aloysius girls imeshika nafasi ya nane na shule ya sekondari ya Wavulana ya Marian yenyewe iko katika nafasi ya tisa.

Nafasi ya 10 kwa shule kumi zilizofanya vizuri mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka 2020 imeshikiliwa na shule ya sekondari ya St Augustine Tagaste.