Wajue Wanafunzi 10 waliofanya vizuri mtihani wa kidato cha nne

0
148

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne, huku Wavulana wakiongoza katika orodha ya Wanafunzi 10 bora.

Katika orodha ya Wanafunzi 10 bora, Wavulana wapo saba na Wasichana ni watatu.

Kwa mujibu wa matokeo hayo yaliyotangazwa na Katibu Mtendaji wa NECTA mbele ya Waandishi wa habari jijini Dar e salaam, Paul Luziga wa shule ha sekondari Panda Hill ameshika nafasi ya kwanza akifuatiwa Justina Gerald wa shule ya sekondari ya Canossa.

Timothy Segu kutoka shule ya sekondari ya Mzumbe ameshika nafasi ya tatu, Isaya Rukamya wa Feza Boys nafasi ya nne, nafasi ya tano imeshikwa na Ashraf Ally kutoka Ilboru na Samson Mwakabage kutoka Jude ameshika nafasi ya sita.

Nafasi ya saba yupo Derick Mushi kutoka shule ya sekondari Ilboru, nafasi ya nane ni Layla Atokwete wa Canossa, Innocent Joseph kutoka sekondari ya Mzumbe ameshika nafasi ya tsa na nafasi ya kumi imeshikwa na Lunargrace Celestine wa shule ya sekondari ya Canossa.

Shule ya sekondari ya Canossa ndiyo iliyoongoza kwa kuingiza idadi kubwa ya Wanafunzi katika kumi bora ya wanafunzi waliofanya vizuri kwa kuingiza Wanafunzi watatu