Mwanasaikolojia Dkt Chris Mauki akizungumza na Watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ambao ni Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi jijini Dar es salaam, ambapo ameelezea namna fikra na mitazamo ya watu inavyoweza kuchochea au kukwamisha mafanikio katika kazi.
Dkt Mauki ameeleza pia umuhimu wa kuwa na malengo binafsi na kwamba kukosa malengo binafsi au malengo binafsi kutofanikiwa kunakwamisha utendaji kazi wa mtu.
Ameeleza kuwa mtu anapokuwa na malengo ya chini au anapojiona hawezi, fikra na mtazamo huo unachangia kushindwa kutimiza wajibu wake kwa viwango vya juu kwa sababu hatopenda kile anachofanya.
Ametumia jukwaa hilo kuwashauri Watumishi hao wa TBC kupanua uelewa wao wa mambo kwani dunia inabadilika, hivyo wasikubali kuwa watu wa kujua kitu kimoja tu katika maisha yao yote.