Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Shule ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) wametembelea ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni, kwa lengo.la kujifunza zaidi kuhusu fani ya uandishi wa habari na uzalishaji wa vipindi.
Katika ziara hiyo fupi, Wanafunzi hao wametembelea vitengo mbalimbali vya shirika hilo ikiwemo studio ya kurushia matangazo, kuona namna Watendaji wanavyoandaa vipindi mbalimbali hadi vinapomfikia mtazamaji.
Wanafunzi hao pia wamepata nafasi ya kuzungumza na Waandishi mbalimbali mahiri wa habari wa TBC na kupata ujuzi na mbinu za kuzingatia na kufuata ili kuwa waandishi bora wa habari.
Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt Ayub Rioba Chacha amewataka Wanafunzi hao kuwa Wabunifu kwa kuwa ushindani ni mkubwa ndani ya tasnia ya habari.
“Pamoja na kwamba unasoma ‘degree’ jiongeze. Mimi ninaowatafuta bwana ni wale wanaowagombania, yani ukija kwangu we niambie una kitu gani unakuja kuongeza TBC… kwa sababu uta-add value [utaongeza thamani],” amesema Dkt Rioba.
Mwakilishi wa Wanafunzi hao Mary Kiria amemshukuru Dkt Rioba kwa kuwapa nafasi ya kuitembelea TBC kwa kuwa wamewexa kujifunza mambo mengi.