Wataalam wa masuala ya afya kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) wamewasili huko Wuhan nchini China, kufanya uchunguzi kuhusiana na chanzo cha ugonjwa hatari wa Corona ulioanzia katika eneo hilo.
Timu ya Wataalam hao kutoka WHO itakuwa nchini China kwa muda wa wiki mbili, ambapo pamona na mambo mengine itakuwa na mazungumzo na Maafisa wa Serikali ya China, lengo likiwa ni kuimarisha uhusiano baina ya pande hizo mbili.
Hata hivyo wakazi wa mji wa Wuhan wameshangazwa na ujio wa wataalam hao, kwani maisha katika mji wao yanaendelea kama kawaida, kwa vile watu wengi walikwishapona na shughuli za uzalishaji mali kuanza tena.
Wataalam wa WHO walichelewa kufika nchini China kwa vile kulikuwa na mazungumzo marefu kati ya pande hizo mbili kabla ya kuruhusiwa kuingia nchini humo.