Timu ya Namungo FC imesonga mbele kutinga hatua ya mtoano ya kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho barani Africa
Namungo FC leo wametoka sare ya bao tatu kwa tatu na timu ya El Hilal
Obein ya Sudan na wao kufuzu kwa jumla ya magoli matano kwa tatu baada ya kushinda mchezo wa kwanza hapa nyumbani kwa bao mbili kwa bila
Magoli ya Namungo FC hii leo yamefungwa na Stev Sey aliefunga goli
kwenye dakika ya mbili ya mchezo mengine yatiwa kimiani na Bilimana Blaise na mlinzi wa kushoto Edward Manyama akafunga goli la tatu
Sasa Namungo FC maarufu kwa jina la wauaji wa kusini wanasubiri timu
itayotolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ili wapambane nayo
kuwania kufuzu hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho.