Meli mpya ya MV Mbeya II yaanza rasmi safari zake  

0
129

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua rasmi safari za meli mpya ya MV Mbeya II itakayotoa huduma katika ziwa Nyasa nchini na nchi jirani za Msumbuji na Malawi.
 
Meli hiyo yenye thamani ya shilingi bilioni 9.1 ni muendelezo wa Serikali wa kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji wa mizigo na abiria, kwa lengo la kuboresha uchumi.
 
Waziri Mkuu Majaliwa amezindua safari za meli hiyo katika bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa mkoani Ruvuma na kuwataka Wananchi waitunze meli hiyo ambayo imejengwa na kampuni ya Kitanzania ya Songoro Marine.
 
Amesema Tanzania imezungukwa na nchi nane ambazo zinategemea kupata bidhaa mbalimbali kutoka nchini, hivyo Wananchi watumie fursa ya uwepo wa meli hiyo kufanya biashara.
 
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Majaliwa, Wananchi hawawezi kupata maendeleo bila ya Serikali kujenga miundombinu kama ya meli, barabara, bandari, hivyo amewataka waitumie vizuri kwa ajili ya kukuza uchumi wao.