Ridhiwani Kikwete ahani msiba wa mtoto wa Nyerere

0
110

Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani, -Ridhiwani Kikwete amefika nyumbani kwa familia ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Msasani jijini Dar es salaam kuhani msiba, kufuatia kifo cha Rosemary Nyerere aliyefariki dunia Januari Mosi mwaka huu jijini Dar es salaam.

Ridhiwani Kikwete pia ameweza kusaini kitabu cha maombolezo na kutoa pole kwa familia ya Nyerere wakiwemo Watoto na Wajukuu.

Awali akitoa pole kwa mtoto wa Hayati Baba wa Taifa, – Makongoro Nyerere, Ridhiwani Kikwete ameeleza kuwa familia ya Nyerere imepata pigo kubwa kufuatia kifo cha Rosemary, hivyo anaungana na familia hiyo katika oipindi hiki cha majonzi.

“Tunaungana kwa pamoja katika msiba huu mzito hakika umetugusa sote, kwa niaba ya familia yangu pamoja na Wanachalinze tunatoa salamu za pole kwa Wanafamilia ya Nyerere,” amesema Ridhiwani Kikwete.

Rosemary alikuwa miongoni mwa watoto saba wa Mwalimu Nyerere.