Heri ya siku ya kuzaliwa Jenerali Mstaafu David Msuguri

0
221

Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa Shujaa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali David Msuguri, ambaye alikuwa  Mkuu wa Majeshi wa Tanzania kati ya mwaka  1980 hadi mwaka 1988.

Jenerali Mstaafu David Msuguri ametimiza umri wa miaka 101 ambapo yupo Musoma mkoani Mara akiendelea na shughuli zake za kila siku.
 
Alizaliwa Januari 4 mwaka 1920 huko Butiama, na pia alifahamika kwa jina la Jenerali Mutukula.

Jenerali.Mstaafu Msuguri alikuwa miongoni mwa Makamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliokuwa mstari wa mbele katika vita ya Kagera dhidi ya Nduli Iddi Amin Dada wa Uganda mwaka 1978.
 
Hii ilitokana na Iddi Amini kuvamia eneo la Kyaka – Kagera na kudai eneo hilo ni sehemu ya Uganda.
 
Heri ya siku ya kuzaliwa Jenerali Mstaafu David Msuguri na hongera kwa kutimiza umri wa miaka 101.