Makamu wa Rais awajulia hali majeruhi wa ajali ya treni

0
183

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewajulia hali majeruhi wa ajali ya treni iliyotokea hapo jana katika eneo la Kigwa wilayani Bahi mkoani Dodoma wanaoendelea kupatiwa matibabu ķatika hospitali ya General.

Akiwa hospitalini hapo Makamu wa Rais amesema kuwa, Serikali ipo pamoja nao na inawaombea wapone haraka na kwamba itahakikisha wanapata matibabu pamoja na huduma nyingine zote wanazostahili.

Ameupongeza uongozi wa mkoa wa Dodoma chini ya mķuu wa mkoa huo Dkt Binilith Mahenge kwa kuhakikisha wanachukua hatua za haraka za kuwasaidia watu wote waliopata ajali.

Pia amewapongeza Madaktari wa hospitali zote za mkoa wa Dodoma, Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano wao katika kuwasaidia majeruhi wa ajali hiyo.

Watu watatu wamethibitika kufariki dunia katika ajali.hiyo na wengine zaidi ya sitini kujeruhiwa.

Wakati ajali hiyo inatokea, treni hiyo ilikuwa na watu 720.