Manchester United kuikaribia Liverpool kileleni

0
148

Ligi kuu England umechezwa mchezo mmoja baada ya mchezo wa Tottenham dhidi ya Fulham kuhairishwa kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona kwa wachezaji.

Timu ya Liverpool imevutwa shati na Newcastle united baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana mchezo ambao Newcastle walikuwa nyumbani.

Kwa matokeo hayo Liverpool anafikisha alama 33 katika msimamo wa ligi hiyo na iwapo Manchester atashinda mchezo unaofuata atakuwa alama sawa na bingwa mtetezi.